'Malaika' anayelipa madeni ya wagonjwa hospitali

Zeal Akaraiwai
Nchini Nigeria ,ni nadra sana kwa huduma za afya kutolewa bila malipo hivyo kama mtu huwezi kulipia huduma hiyo basi hataruhusiwa kuondoka katika kituo hicho cha afya baada ya kuhudumiwa.
Swali linakuja kuwa ni: Nani anaweza kusaidia? Katika jamii ambayo ina imani kubwa ya kidini , wagonjwa wengi ambao hushindwa kulipia huduma hiyo ya afya wanabaki na matumaini kuwa Mungu ataonesha njia ya kuwasaidia.
Zeal Akaraiwai ni malaika ambaye hana mabawa kama tunavyofahamu malaika walivyo bali yeye ana gari la kifahari la aina ya Benzi lenye rangi nyeusi.
Yeye huwa anatembelea hospitali za serikali mjini Lagos na anapofika huwa anasalimia watu wa ustawi wa jamii na kuomba majina ya watu ambao wamepona vizuri kurudi nyumbani lakini wanashindwa kuondoka kwa sababu hawajawezi kulipa deni lao la huduma ya afya.
The list
Zeal alikutana na baadhi ya watu ambao wameshindwa kuondoka hospitalini hapo kwa takribani wiki 6 hadi 8, baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Baadhi ya hospitali za Nigeria ilikuepo mipango ya kulipia kabla kwa wale watu ambao wana kipato kidogo au hawana kabisa.
Zeal Akaraiwai and hospital social workers
Wafanyakazi wa ustawi wa jamii huwa wanamuongoza Zeal kwa wagonjwa na huwa anazungumza nao kwa upole na kuuliza nini ambacho kimewasibu mpaka wamefika hospitalini hapo.
"Ni namna gani utaweza kulipia deni lako la hospiali?" Zeal alimuuliza mmoja wa wagonjwa na mgonjwa huyo akajibu " Ninamuomba Mungu atanisaidia".
Zeal alizungumza na mgonjwa huyo kwa muda na mgonjwa huyo hakumuuliza Zeal ni nani na wala Zeal hakumwambia yeye ni nani?
Baada ya mazungumzo yao ,Zeal alienda kulipia deni la mgonjwa huyo ambalo lilikuwa dola 250 na kumfanya mgonjwa huyo kuwa huru kuondoka hospitalini hapo.
Zeal huwa habaki na mawasiliano na mtu yeyote ambaye anamsaidia na huwa hataki hata kuambiwa Asante.
Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinatoa simulizi ya huyu mtu na siku moja watu watasimulia habari zake kuhusu namna ambavyo mwanaume huyo anavyotembelea hospitalini na watu kuamini kuwa malaika alikiuja kulipa madeni yao hospitalini na kuondoka.
"Ndio maana mradi huu nauita Malaika, nikimaanisha kuwa malaika ambaye unatumainia kukutana naye" Zeal alieleza.

Kulipia gharama ya huduma ya afya kwa wagonjwa walioshindwa kulipa ndio namna moja ambayo Zeal anaitumia katika imani yake ya ukristo.
Anasema anataka kuwaonesha watu kuwa kila mtu anaweza kufanya kitu na kumsaidia mtu mwingine.
Marafiki zake Zeal pamoja na familia yake huwa wanamchangia fedha katika mradi wake na yeye huwa anatunza risiti pamoja na maelezo ya mgonjwa ambaye amemlipia hospitali.
Katika wodi ya wanawake, Zeal alienda kuona mwanamke ambaye alikuwa na umri wa miaka 60 ambaye alikuwa hajiwezi na hata amewekewa mashine ya upumulia.
Mwanamke huyo alikuwa amepooza na wahudumu wa ustawi wa jamii walitaka Zeal amlipia deni lake ili aweze kuhamishwa kutoka chumba cha kawaida na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Zeal Akaraiwai and doctor in white coat
Mtoto wa mama huyo ambaye ni mdogo na hana ajira alikuwa amebaki na bumbuwazi tu na sijue nini cha kufanya ili amsaidie mama yake aweze kupona.
Inavyoonekana hata kama mgonjwa huyo atalipiwa deni aliokuwa nalo , bado hizo ni hatua za awali sana na kama mgonjwa huyo atapona.
Pamoja na kwamba Zeal alizungumza na binti wa mama huyo kwa upole na kumwambia pole.
Ingawa kulipia huduma ya afya ya mama huyo ambaye yuko mahututi kunaweza kwenda kinyume na sheria ambazo amejiwekea mwenyewe, Kwa sababu lengo lake sio kusaidia mtu yeyote ambaye yuko mahututi au anayeendelea kupata huduma.
Mradi wake umelenga kuwalipia wale wote ambao wamepona na wako tayari kurudi nyumbani lakini hawawezi kutokana na kukosa fedha ya kujikomboa kutoka hospitalini baada ya kupata huduma.
Ingawa kuna wakati huwa hakubaliani na hayo, Zeal alisema.
A baby lies in hospital with a bible, left by the mother, open to read at one end of the bedHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMtoto akiwa amelala pembeni ya biblia katika hospitali moja huko Lagos
"Ninakumbuka kuwa kuna mwanamke aliyelazwa hospitalini kwa miezi 11 na nilimlipia dola 400 ili afanyiwe upasuaji.
na leo nimetembele hospitali hii ya umma kuna zaidi ambayo ninahitaji kuyafanya.
'The Angel Project ' mradi wa malaika uliamua kumlipia mgonjwa wa upasuaji wa mguu na Zeal alitaka kujua hali ya mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 10 unaendeleaje.
Mpaka sasa amelipia huduma ya mtoto huyo na anaendelea kulipia huduma ya mtoto huyo mpaka atakapondoka nyumbani.
Zeal aliwahi kukutana na binti huyu mdogo lakini sasa hataki kumuona tena na anachokumbuka kuwa mtoto huyo ana macho ambayo yanafanana na ya mtoto wake.
Zeal anapitia majina ya kila aliyeko katika orodha ya ustawi wa jamii, na kumlipa mweka hazina wagonjwa nane.
Mara zote utaratibu uliopo hospitalini huwa unampa huzuni na anachukia kwa kile ambacho serikali inashindwa kukifanya.
Haoni sababu inayopelekea watu kushinwa kuwa na bima za afya zinazoeleweka.
Kuna watu makini ambao wanaweza kuangalia namna gani mpango wa huduma ya afya unaweza kufanikiwa.
Zeal Akaraiwai
Nchini Nigeria ni asilimia tano tu ya watu waliomo nchi humo wana bima ya afya.
Kuna mtazamo tofauti wa namna watu wanaangalia dunia inavyofanya kazi, mamilioni ya watu masikini kuweza kulipiwa na serikali .
Lakini Zeal bado ana subira ingawa kila wiki anaona kuwa kuna umuhimu wa watu kuwa na bima za afya.
Watu wanakufa lakini ni wapi tunaweza kuweka gharama ya maisha ya binadamu.
CHANZO:BBC SWAHILI

Post a Comment

Previous Post Next Post