Magonjwa hatari 10 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi.
Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:
1. UGONJWA WA MOYO
Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.
Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.
2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili.
Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.
3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA
Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho.
Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.
4. KINGA YA KISUKARI
Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia.
Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na ‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.
Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.
5. DAWA BORA YA USINGIZI
Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’.
Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’ mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini.
Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.
Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu.
6. DAWA BORA YA UVIMBE
Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation).
Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.
Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu.
Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.
7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3. Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.
8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME
Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.
Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic hyperplasia’.
Wanaume kazi ni kwenu.
9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.
Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili.
Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia
Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako.
Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.
10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)
Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya msongo wa mawazo kiafya.
Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.
Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance).
Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’.
Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.
11. Huzuia mchanga kwenye kibofu cha mkojo
Faida nyingine ya kushangaza kuhusu mbegu za maboga kiafya ni ule uwezo wake wa kuzuia mchanga au mawe kwenye kibofu cha mkojo.
Kinachofanya hili liwezekane kupitia mbegu hizi ni kule kuwa na kiasi kingi cha ‘phosphorous’ ambayo ni msaada mkubwa katika kuzuia mawe au mchanga kujilundika katika kibofu cha mkojo.
Pia unashauriwa kuwa unakunywa maji mengi kila siku ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili.
12. Huimarisha afya ya mifupa
Kadri umri unavyoongezeka ndivyo na uwezo na uimara wa mifupa yako unavyopungua. Imefahamika sasa kuwa madini ya kalsiamu peke yake siyo kitu kinachoimarisha afya ya mifupa.
Kuna madini na vitamini vyngine mhimu ili kuimarisha afya ya mifupa. Mbegu za maboga ni chanzo kizuri sana cha magnesiamu, Zinki, Vitamini K na viinilishe vingine vingi mhimu katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
13. Zinasaidia kuweka sawa shinikizo la juu la damu
Shinikizo la juu la damu ni moja magonjwa sababishi ya vifo kwa watu wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo. Mbegu za maboga ni kitu mhimu kuongezwa katika mlo kwa watu wote wanaosumbuliwa na shinikizo la juu la damu.
Mbegu za maboga zina kiasi kidogo cha sodiamu na zina kiasi kingi cha potasiamu na magnesiamu vitu viwili mhimu katika kuweka sawa shinikizo la damu mwilini.
14. Zinaimarisha afya ya ubongo 
Kadri unavyoendelea kukua ndivyo na uwezo wa ubongo wako unavyopungua. Hata hivyo bado unayo nafasi ya kuzuia hilo kama utaishi na kula vizuri.
Mbegu za maboga asidi mafuta ya Omega 3 zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘alpha-linolenic acid’ ambazo ni mhimu sana katika kulinda na kustawisha afya ya ubongo.
Vyakula vyenye Omega-3 husaidia kupunguza kasi ya seli za ubongo kuzeeka wakati huo huo vikizuia uharibifu wa seli za ubongo kutokana na vijidudu nyemelezi katika ubongo.
15. Zinaweka sawa Ph ya mwili
Mwili unaweza kuwa katika hali mbili, ama katika asidi au katika alkaline (Ph). Mwili unapokuwa na asidi nyingi ndipo unapopatwa na magonjwa mengi kirahisi zaidi. Magonjwa hayo ni pamoja na maumivu ya mifupa, saratani, kisukari, vidonda vya tumbo, kichwa kuuma nk
Hivyo ni mhimu chakula chako kiwe kwa sehemu kubwa ni chakula chenye alkalini na si asidi (tindikali) ili kukusaidia ubaki na Ph (Potential Hydrogen) ya 7.4 mara nyingi. Kumbuka chochote chini ya 7 Ph ni asidi.
Mbegu za maboga ni moja ya vyakula vizuri zaidi vyenye alkalini ambavyo unatakiwa kuvijumuisha kwenye mlo wako.
16. Zinatibu tatizo la upungufu wa damu
Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma hivyo kuwa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na upungufu wa damu unaosababishwa na kupungua kwa madini ya chuma.
Tafiti zinasema kula vyakula vyenye madini ya chuma kila mara kunasaidia kuongeza madini ya chuma kwa watoto, vijana, wanawake wanaonyenyesha na kwa wamama wajawazito. Hili linazifanya mbegu hizi kuwa msaada mkubwa kwa wale wanaopata tatizo la upungufu wa damu unaotokana na kupungua kwa madini ya chuma mwilini.
17. Zinasaidia kupunguza uzito wa mwili
Weka pembeni vyakula vyenye sukari nyingi na badala yake tafuna mbegu za maboga. Kinachotokea hapa ni kuwa mbegu hizi zinao uwezo wa kukuacha ukijisikia umeshiba kwa kipindi kirefu na hivyo kukuondolea hamu ya kutaka kula vyakula vingine feki.
Nyuzi nyuzi nyingi katika mbegu hizi zinazifanya kuwa chakula kizuri kuongezwa kwenye chakula chako cha asubuhi.
Hata hivyo sababu zina protini nyingi iwapo utazidisha kula unaweza kuongezeka uzito na unene badala ya kupungua hivyo uwe makini.
18. Zinarahisisha uponyaji wa vidonda 
Mbegu za maboga pia ni msaada mkubwa kwa watu wenye vidonda kwa kuwa zinafanya kazi ya kuponya vidonda kuwa rahisi zaidi sababu zina vitamini A na madini ya zinki kwa wingi.
Kiais kingi cha vitamini A kwenye mbegu za maboga kinaweza kuwa msaada kuhamasisha uponyaji wa vidonda kwa mjibu utafiti mmoja uliofanywa na jarida moja la chuo cha afya ya ngozi nchini Marekani ‘Journal of the American Academy of Dermatology’.
Kwa mjibu wa utafiti, vitamini A ndani ya mwili inaweza kuvutia mfumo wa mwili kujiripea wenyewe ndani kwa ndani bila kuhitaji dawa.
Kama unasumbuliwa na vidonda au kidonda kwa muda mrefu hebu weka mazoea ya kutumia mbegu za maboga mara kwa mara na hutachelewa kuona uponyaji ukifanyika. Hii ni kweli ukizingatia pia mbegu hizi zinaongeza sana kinga ya mwili.
Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.
nutritional-facts-pumpkin-seeds

Post a Comment

Previous Post Next Post